KUHUSU MKUTANO
Huku mizozo ikiendelea katika sehemu mbalimbali za dunia, Benki ya Dunia inashiriki kuchukua hatua madhubuti za kukomesha umaskini ulimwenguni. Mpango wa Taasisi ya Kimataifa wa Benki ya Dunia unayoshughulikia Maendeleo (IDA) ni muhimu katika kufanikisha dhamira hiyo. Ikifanya kazi na washirika kote ulimwenguni na kwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha, IDA inashughulika kutoa suluhu kwa kiwango kikubwa na kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.
KUHUSU IDA20
Mfuko wa maendeleo wa Benki ya Dunia uitwao IDA unafadhili nchi zenye kipato duni duniani. Kupitia ufadhili wa mzunguko wake wa 20 (IDA20) wenye thamani ya dola bilioni 93 (Kwa Kipindi cha Julai 1, 2022 - Juni 30, 2025), IDA imedhamiria kusaidia mataifa maskini zaidi duniani katika safari ya kuelekea upatikanaji wa maendeleo ya kijamii, kibinadamu na kiuchumi.
FAHAMU ZAIDI: Mkutano wa IDA20 – Tathimini Muhula Wa Kati
Mada Maalum
- Mabadiliko ya Hali ya Hewa
- Udhaifu, Migogoro na Vurugu
- Jinsia na Maendeleo
- Mtaji wa Binadamu
- Ajira na Mabadiliko ya Kiuchumi
Masuala Yasiyo na Mipaka
- Kujiandaa kwa Mgogoro
- Madeni
- Utawala na Taasisi
- Teknolojia